Wednesday, October 16, 2013

MAPENZI YA OFISINI HUVURUGA SAIKOLOJI YA MTU.

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.

Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.

Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi kimoja kikubwa sana.

Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa sana.

Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.

Tuesday, October 8, 2013

NJIA ASILIA ZA KUPUNGUZA UZITO:



Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.

NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:

1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.

2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.

3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.

4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.

5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.

6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.

7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).

8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.

9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.

10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia kupunguza uzito.

Maneno Yajengangayo na Kubomoa mahusiano.


Maneno ndiyo hubomoa na kujenga uhusiano.
Hatari iliyopo ni kuwa wanaume wengi wanapowazoea wapenzi wao, hushindwa kutamka neno hilo lakini mwanamke hupenda kusikia akiambiwa hivyo.
Mwambie mpenzi wako jinsi unavyompenda, mthibitishie kuwa mapenzi yako kwake ni makubwa kupita kiasi.
VIPI KUHUSU WANAUME?

Wanawake wengi hulalamika kuwa wanaume ni watata kwenye mapenzi.
Hulaumu kwamba ni ngumu kubaini vitu ambavyo wanaume huhitaji kutoka kwa wanawake.
Wanadai kuwa wakati mwingine hujitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanawapa furaha lakini wanaume huwa hawana hata msisimko.
Hapa chini, nimekuandalia vitu ambavyo wanaume huhitaji kwa wanawake wao. Moja kwa moja, mambo yakienda chanya huwa ni zaidi ya chombezo na hupagawa.
MAPENZI (Love)
Siku zote wanaume huangalia mapenzi kwa wenzi wao.
Mara nyingi wanaume huwa wepesi kuonesha mapenzi kwa wanawake wao lakini ndani ya nafsi zao, hutegemea mambo mengi kama malipo (return) ya upendo waliotoa kabla.
Wanapenda, kwa hiyo nao huhitaji kupendwa ili waone mambo yanakwenda sawa.
Wanawake wengi huwa wanaficha hisia za kupenda, hili huwaumiza wenzi wao.
Onesha mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.
MVUTO (Attractiveness)
Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana kwa wanawake kwa kushindwa kutambua mvuto wao, unavyoweza kuwa kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu.
Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote.
Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.
UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100.
Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe.
Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao.
Jiamini kisha uwe muaminifu.
Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.
FAMILIA (Family)
Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo.
Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja.
Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.
UKARIMU (Kindness)
Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu. Jitazame na ujitengeneze kuwa hivyo ili umvutie mwenzi wako.
Ukorofi, ubishi na roho mbaya siyo sifa ya kike.
UCHESHI (Funny)
Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.
U-MWANAMKE (Femaleness)
Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake.
Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Huhitaji wanawake wanaotimiza wajibu wao kama wanawake kulingana na jamii inavyotambua. Hupenda wanawake wanaojali, kujiheshimu na kadhalika.
Wale walevi hukosa sifa ya u-mwanamke ambayo wanaume huihitaji.

Ndoa na Uaminifu


Uaminifu ndani ya ndoa hujenga familia bora!!! Yes tumekutana tena kwenye kona hii ya
Mapenzi na Uhusiano.
Kama inavyojulikana wazazi wawili ndiyo muongozo
wa familia, baba akiwa kichwa cha familia akifuatiwa
na mama. Siku zote familia bora hutegemea
muongozo mwema wa wazazi, kwani wao ndiyo walimu wa kwanza kwa mtoto. Siku zote watoto hujifunza kupitia wazazi wao
wanachokifanya ili nao wakitumie kama dira ya
maisha yao pindi wakifikia umri wa kujenga familia
zao. Kama muongozo utakaowafanya waweze
kuishi muda mrefu katika maisha ya ndoa na kifo
pekee ndicho kitakacho watenganisha. Katika maisha ya kila siku ya mwanadamu
hawawezi kuishi kama malaika, ipo siku wanaweza
kukosana kwani makosa ni sehemu ya maisha ya
mwanadamu. Ndiyo maana tumefundishwa
kusamehe au kuomba msamaha pale unapojua
umekosa. Lakini kuna baadhi ya familia zimekuwa
zikiwashirikisha watoto wao katika matatizo yao
pindi wakosanapo, ikiwamo kufokeana mbele yao
pindi wazazi wanapo tibuana. Mnashindwa kutafuta sehemu ya faragha na
kuonyana kiutu uzima, kama wazazi ambao siku
zote watoto hutakiwa kujifunza mazuri kutoka
kwenu. Kufokeana mbele ya watoto mnawafundisha
nini? Inapotokea baba au mama anapokuwa akimtumia
mtoto wake kujua kama mwenzake kuna kitu kibaya
amefanya kwa kumuuliza: “Ulipotembea na baba
yako hakuzungumza na wanawake?” Au baba
kukuuliza “Nilipokwenda kazini mama yako alitoka
au alizungumza na mwanamume?” Nina imani kwa mawazo yenu unajiona mpo sawa
kumbe sivyo, kwa mtindo huu inaonyesha ndani ya
uhusiano wenu hakuna uaminifu. Hamuwezi
kumfanya mtoto kama mlinzi wa mmoja wenu. Hivi
mnamfundisha nini au ndiyo mnajionyesha jinsi gani
msivyo aminiana. Kwani mtoto huamini matatizo ndani ya familia ni
msiba mzito ambao mwisho wake ni wazazi
kutengana na kuweka mpasuko katika maisha yake.
Mzazi mwenye busara siku zote hukanyana sehemu
ya faragha ambayo humfanya mtoto aamini siku
zote wazazi wake hawana matatizo. Pia kama una wasiwasi na mwenendo wa
mwenzako kwa nini usimwite mkae chini na kutatua
kwa busara, kwani hakuna mwanadamu
aliyekamilika asilimia mia. Familia bora ni ile ambaye inahakikisha matatizo
yao hayaathiri watoto wao, hutatua kwa busara huku
wakizingatia watoto wao wanawategemea wao.
Wazazi kuweni walimu wema katika familia zenu ili
kujenga familia yenye maadili mema.

Mambo 10 ya kufanya kabla hujatimiza miaka 26

.
1. Jifunze kuweka akiba ya
fedha na iache bila kuigusa
gusa.
2. Tafuta mpenzi sahihi na
tulia naye, panga maisha.
3. Ishi mahali pa peke yako,
acha kuishi kwenye nyumba
au kupanga na washkaji.
4. Lipa madeni yako ya
zamani. Yote!
5. Tengeneza mwili ambao
unataka halafu jitahidi ku-
umantain! Anza kuzingatia
kuishi kwa kujali afya yako
sana.
6. Jitahidi uwe na marafiki
ambao wana changamoto za
kimaendeleo
zitakazokusaidi a.
7. Anza kujinunulia assets
kama ardhi na nyinginezo.
8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa
heshima, si tu ilimradi
umependeza.
9. Kubali sasa kwamba
umekua na acha tabia na
mambo ya kitoto
10. Yaache ya zamani yapite
na anza mapya. kama akina Mwajuma,hawa,na kinaflani flani
huna mpango nao, achana
nao. Acha kurudi rudi nyuma!

Sunday, October 6, 2013

Jumbe za Malavidavi

Kila ninapowaza kwanini nilikupenda wewe sipati jibu, kila siku nafikiria zawadi ya kukupa kuonyesha mapenzi yangu kwako nakosa. Tambua kitu kimoja lahazizi wangu, nakupenda sana!
*****
Though Shakespeare is great , he'll never find the right words to describe u because he simply never xperienced knowing a wonderful person like u, friend!
*****
Fumba macho sweetie, haya fumbua, soma neno linalofuata…nakupenda na kamwe sitakusaliti milele!
*****
If I could change the alphabet, I would put U and I together!
*****
Kila kitu ulichonacho kinanipa mshawasha, macho yako mazuri, tabasamu tamu na umbo lako zuri, lakini kubwa zaidi ni mahaba yako mazito!
*****
I knew u've got plenty of frens. Some r old, some r new. Some r false, some r truth. I may not be ur perfect fren but one thing I will always be - d cutest u've got.
*****
Mpenzi wangu, natambua kuwa unanipenda kwa dhati, nimekuficha moyoni mwangu, nakuomba unihifadhi moyoni mwako nijifiche, nisipatwe na mvua wala jua!

Kwa wapendanao

UNAPOKUWA KATIKA UHUSIANO WA KIMAPENZI, KWA HAKIKA UNAPASWA KUULINDA UHUSIANO WAKO KWA GHARAMA YOYOTE.
WATAALAMU WA MAMBO YA MAHUSIANO WANAAMINI UJUMBE WA MAPENZI HUDUMISHA PENZI KWA KIASI KIKUBWA SANA. LEO NIMEKUANDALIA MESEJI KALI ZA KIMAPENZI KWA AJILI YA KUMTUMIA UMPENDAYE, LENGO LIKIWA NI KUBORESHA PENZI LAKO. KAZI KWAKO KUCHAGUA MOJA NA KUMTUMIA LAHAZIZI WAKO!
I am opening an emotional bank account for u sweetheart, so deposit your love
in it and you will get the interest!
*****
Wewe pekee upo moyoni mwangu, nitaendelea kukupenda siku zote za maisha yangu! Katika siku hii ya wapendanao, wewe ndiyo ua la moyo wangu!
*****
If I could die early I would ask God if I could be your guardian angel, so I could wrap my wings around you and embraces you whenever you feel alone...
*****
Najua kuna vishawishi vingi sana uko ulipo, lakini nikiwa moyoni mwako, siku hii itakuwa nzuri zaidi kwetu, tupendane daima lahazizi…
*****
It is hard to talk when your in love because when I look into your beautiful I get my breath taken away…
*****
Midomo yako inanichanganya, macho yako yananivutia, umbo lako linaniacha hoi, wewe ni wangu wa ubani siwezi kudanganywa na walaghai…
*****
Penzi langu kwako ni la milele, nitakuhifadhi moyoni mwangu siku zote za maisha yangu, uwe wangu nami niwe wako daima, nakupenda dear…
*****
R. for red , red for blood , blood for heart, heart for love, love for you, you for me, me is you , I love you ma’ dear!
*****
Hiki ni kipindi muhimu kwetu, kuoneshana mapenzi ya kweli, wanafiki wabaki kimya kwa aibu zao…
*****
I’ll drop a tear drop into the ocean n the day I find that tear drop is the day
I stop loving u!
*****
Usiku wa jana ulikuwa wa aina yake, ulinipa mambo matamu yasiyo ya kawaida, ulinifurahisha sana mpenzi wangu, ulidhihirisha kuwa wewe ni kidume uliyeubwa kwa ajili yangu..
*****
Baby I have an addiction problem, people say I should go to rehab but I
always tell them I don’t wanna go cause I’m addicted to ... YOU
*****
Kutokana na penzi la siku ya kwanza kwako, bado ninatamani kuendelea kujificha katika moyo wako, wewe ni taa ya maisha yangu, nahitaji uwe nami siku zote, nami nitakuwa nawe, hadi kifo kitapotutenganisha! Hii ni ahadi ambayo sitaivunja hadi siku naingia kabuni, tupendane mpenzi…

Sindano kali za maloveee......

OMBA MSAMAHA KWA MPENZI WAKO:
Mpenzi wangu naomba unisamehe, nakupenda sana dear na ni kweli kuna wakati nakukosea, lakini amini nakupenda. Sijawahi kujuta na sitajuta kamwe kuwa na wewe! Naamini nitaendelea kuwa mwaminifu kwako, sio leo tu, bali siku zote za penzi letu!
*****
Tukae kimya sheteni apite, naamini haikuwa akili yangu bali ni ushawishi wa sheteni ambaye siku zote amekazania kuharibu penzi letu!
*****

Wewe kwangu ni kila kitu, sipendi kuyaona machozi yako mpenzi wangu! Sogea nikufute na unirudishe tena mikononi mwako, nakupenda sana dear!
*****
Wewe ni taa kwangu imulikayo gizani, nakupenda sana mpenzi wangu wa moyo, utakuwa wangu siku dear! Kosa nililofanya ni kwa bahati mbaya, naomba unisamehe na ninaahidi kutorudia tena katika penzi letu!
*****
Tega sikio dear, nakupenda sana, ukweli wa ile sms uliyoifuma kwenye simu yangu, haikuwa yangu bali mtumaji alikosea kwa bahati mbaya! Nipo tayari tumpigie tukiwa pamoja tumuulize, kweli niamini dear! Naomba usiniache maana maisha yangu bila wewe ni sawa na giza nene!
****


Mimi kwako ni kipofu, nishike mkono tuvuke barabara, magari ni mengi na yanapita kwa kasi, siwezi kuona zaidi ya kusikia yakiunguruma, honi za magari siwezi kupima umbali wake, usiniache katikati ya barabara nitagongwa na kufa mara moja! Njoo niokoe nitagongwa mpenzi wangu! Forgive me dear...

Utendee haki moyo wako, usilazimishe mapenzi!

Leo nimekuja na mada nyingine, kama kawaida ni mada nzuri itakayokupa ufahamu mpya juu ya maamuzi yako yahusuyo mapenzi. Hivi ni kweli kwamba unautendea haki moyo wako? Mpenzi uliyenaye unampenda au unajilazimisha tu kuwa naye?
Somo la leo litakupa mwanga wa kujua haki ya moyo na tamaa za mwili wako ni kipi sahihi kutendewa haki. Elewa kuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi. Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haklupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi! Kama ndivyo, kwanini uwe mtumwa?
Unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!
Mapenzi ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako! Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!
Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!
Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu!
Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. Hii inaama kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha!
KUJIFUNZA KUPENDA!
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. Hufanya hivyo ajidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo.
"Pesa anazo, magari anayo, hata kama simpendi nitajitahidi kumpenda taratibu," baadhi ya wasichana huwaza hivi. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa.
MADHARA
Yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi wako uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndio msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote.
Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea? Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza kukua.
UNATENDA HAKI?
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaewza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.
Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo. CREDIT KWA JOSHUA

TURUDI CHUMBANI: Mambo yatakayokufanya uonekane bora kwa mpenzi wako muwapo chumbani.


Wapenzi ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.

Inawezekana wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa huna thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele 10 vifuatavyo, nina imani utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi na zaidi.

1. MWANZO WA PENZI
Siku zote nimekuwa nikisisitiza kuwa, jinsi unavyoanza ndivyo utakavyomaliza! Kama ulianza vibaya uhusiano wako tegemea kumaliza vibaya, lakini kama

Kama unatarajia kuingia katika uhusiano na mpenzi mpya hakikisha hujionyeshi tofauti na hali yako halisi ilivyo! Jifunze kujikubali, hata kama unafanya kazi ambayo unadhani ni hadhi ya chini, mbainishe mpenzi wako hali halisi ilivyo. Kama anakupenda, kazi yako haiwezi kupunguza mapenzi baina yenu.

Ikiwa ndiyo kwanza mnaanza uhusiano, zingatia hili, na kama mpo katika uhsiano kwa muda mrefu ukagundua wazi kuwa kuna mahali ulikosea, anza kufanya mabadiliko kuanzia sasa. Bado hujachelewa, mwambie ukweli naye atakuheshimu kutokana na ukweli wako.

Kudanganya hakuna mantiki, kudanganya ni utumwa, usikubali kuingia katika utumwa au kifungo cha aina hiyo. Ukweli ni silaha ya kwanza katika mapenzi, anza hivyo kuanzia mwanzo na kama ulikosea, ulijisahau au hukujua, basi anza leo!

2. USIJICHUKIE
Itakuwa kichekesho kama utasema unampenda mpenzi wako wakati wewe mwenyewe hujipendi! Huwezi ukasema unamthamini mpenzi wako wakati thamani yako mwenyewe huitambui.

Naamini tunakwenda sawa, kama unashindwa hata kuoga na kubadilisha nguo safi nani atakayekupenda? Huwezi kuwa wa kisasa kama huzingatii usafi, hakuna atakayevutiwa na wewe kama wewe hutaki kujivutisha. Sio ajabu mpenzi wako akakutosa kwa sababu tu huna muonekanano mzuri kwa rafiki zake.

Nani atakayekupenda wakati wewe mwenyewe huonyeshi kama unajitambua?
Jikubali, jithamini! Kuwa msafi wakati wote, kauli zako ziwe safi siku zote mpenzi wako atakuwa huru kuwa na wewe. Isifikie hatua mpenzi wako akataka kutoka na wewe lakini akasita kwasababu hajui ukija utakuwa umevaa nguo za namna gani. Upo hapo?

3. MWONEKANO WAKO
Mwonekano wako unaweza kukuanisha jinsi ulivyo kwa wanaokutazama, wakati mwingine inawezekana ukatafsirika tofauti na ulivyo kutokana na jinsi unavyovaa na tabia zako zingine!

Lazima uwe kijana wa kisasa, kwa kuzingatia hilo unapaswa kuwa makini kwa kila kitu kinachoonekana kwa wanaokutazama. Jenga mazoea ya kutambua aina ya nguo na mahali ulipo, usivae nguo za ufukweni ofisini au nguo za mtaani ukavaa ofisini!

Wanaokuangalia wanapata taswira ya jinsi usivyo makini au makini kutokana na mavazi yako. Vaa nguo safi kila wakati, labda kama unafanya kazi ambayo inakulazimu kuwa mchafu, ila baada ya hapo unapaswa kuwa msafi. Ukizingatia hili utamfanya mpenzi wako afurahie kuwa na wewe siku zote. Amini popote ulipo, jinsi ulivyo ndivyo anavyoonekana mpenzi wako.
Itaendelea wiki ijayo.
Credit kwa Joseph shaluwa

Friday, October 4, 2013

Jinsi ya kuzuia matiti kuanguka



Hakikisha mpenzi wako anayanyonya akiwa ameshikilia au wewe umeyashikilia, vilevile hakikisha anapo yapapasa au kuyatomasa, basi afanye hivyo bila kuyahangaisha....kwamba ahakikishe yametulia.

Unapokuwa kwenye mkao wowote unaosababisha matiti yako yasumbuke basi hakikisha mpenzi kayakamata sawa au kama wewe mwenyewe hujapoteza akili kwa raha basi yashikilie....kwa kufanya hivyo kutasaidia matiti yako yasilegee kabla ya wakati.

Ni wazi kuwa matiti yanakwenda kulegea pale yatakapokuwa yanapoza homoni yaani yaani mwamke kuzeeka lakini kuzaa au kuwa mdada mkubwa (over 40) sio sababu ya kujiachia

Jifunze jinsi ya Kubusu







Ili mfurahie busu mnatakiwa
kupeana (umbusu-akubusu) hivyo
ni jambo muhimu la kuzingatia ni
kuto achama au kukusanya
midomo yako kama unataka
kubusu kwa sauti (kama zile busu
za sauti za vijana mtaani) na
badala yake busu kimahaba…..
Sogeza midomo yako kama ilivyo
(umeifumba lakini iko-relaxed)
kwenye midomo ya unaetaka
kumbusu…..kisha itulize midomo
hiyo juu yake na sasa toa “busu
kavu” juu ya midomo yake kisha
jitoe alafu rudi tena x3…..1)-inua
uso wake kwa kutumia kidole (hii
ni kwa wanaume) na mbusu moja
kwa moja kwa kugusanisha pua
kiaina…2)-Busu kwa kupindisha
shingo/kichwa ili kutogusanisha
pua zenu…3)-ukiwa umepindisha
kichwa/shingo…mshike mkono
au mkumbatie kiasi na busu tena.
Ukiona/hisi anajisogeza au
anakupa ishara kuwa uendelee
kwa kufungua mdomo kiaina,
kukush
ika mkono/kifua/kitambi/kiuno
au kuweka mkono kwenye bega
basi endelea na “busu nyevu”
kwa kubusu ktk mtindo wa
kulamba-kunyonya mdomo(lips)
wa chini na tulia hapo kwa
sekunde chache kisha pokea
ulimi wake kwa ulimi wako (bila
kuachama…ni mumo kwa
mumo)alafu ukwepe na kisha
rudi kwenye midomo ya busu lip
ya juu…..
Ongeza ujuzi wako sasa…na
kumbuka kupumua kwa kutumia
pua sio unampumulia mwenzio
mdomoni….(atashiba hewa) au
unabada pumzi (Mauti
inakukumba). Unaweza kufumba
macho aku kukodoa....inategema
na wakati wenyewe.
Kuna aina tofauti za kubusu ili
kutuma ujumbe kwa mpenzi
wako lakini busu zote
zinahusiaha ulimi na mate.
Unaweza ukapewa busu wewe
ukadhani ni kawaida (kama hujui)
lakini mwenzio anakwambia
amechoka, anakupenda,
anashukuru, amefurahi kukuona,
hataki kungonoana siku/wakati
huo, hana raha/hujamfurahisha,
anataka kuwa peke yake,
anamachungu, yuko busy n.k.
Busu hizi zina jinsi yake ambayo
utaijua kwa vitendo…..nadhani
wabongo wengi hawajui unless
wamewahi kufanya mahusiano ya
kimapenzi na watu wenye
utamaduni wa kubusu kwa mate/
ulimi (Wazungu wazuri ktk hilo).
Baadhi ya watu hujiuliza kwanini
wazungu wanapigana denda kila
wakati lakini hawadisi/dindishi?
Sio kila denda ni “nataka
kutomabana” kuna denda
nyingine za machungu au hasira,
nakumbuka kama unampenda
mwenzio lazima utahisi
machungu yake sasa kudisa
kutatoka wapi hapo ei?
Ongezea ujuzi na utundu ulionao
ili na wengine wajifunze


MADHARA YA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE

     Habari ndugu mdau wa blog hii,natumaini upo poa na unapendezewa na post zetu,leo tugusie madhara ya kuruka ukuta yaani ngono ya kinyume na maumbile.

Tunapoamua kufanya jambo sio kwamba tunafuata mkumbo au kulazimishwa bali ni our choice.
Kufanya ngono kusiko a.k.a Tigo “MWIKO” katika jamii nyingi Ulimwenguni sio kwa vile tu inamaanika kuwa ni uchafu na inamadhara makubwa ya kimwili, kiakili na kiafya bali ni kinyume na mafundisho ya imani zetu za Dini.

Kinachofanyika chumbani ni uamuzi wenu ninyi wawili mnaopendana ikiwa tu mtakubaliana na kufanya hivo na pia ni siri yako wewe na mpenzi wako, kuna wapenzi wengi tunafanya mambo ya ajabu sana na watu tunaowapenda na tunafurahia na tunazidi kupendana na kutakana zaidi na zaidi kila siku….lakini mambo hayo ni “taboo” ktk jamii kama ilivyo kwa Tigo 

Kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) hujaribu na kisha wanajikuta wanafurahia na hivyo wanaendelea na kuna wengine hutaka kujua “unajisikiaje” lakini wanajikuta hawafurahii au mmoja wao hafurahii na hivyo wanaacha na kutorudia tena tendo hilo la mugongo-mugongo.
Pamoja na kuwa watu kuheshimu miiko ya dini zao, kupinga na kulisema vibaya tendo hili wachunguzi wa mambo ya Tigo wanadai kuwa mwanamke mmoja kati ya wanne anashiriki ngono ya nyuma (sasa hii sijui ni kuridhisha wapenzi au ni wao wanafurahia)…….wazoefu watusaidie hapa.

Ukweli kuhusu Tigo.- Sio tendo asilia ktk swala zima la ngono na mapenzi hivyo kumbuka unapoamua kugawa tako kuwa na uhakika ndio kitu unataka kukifanya na sio kukifanya kwa vile “mchumba” kaomba/anataka…..wewe ndio mwenye maamuzi makuu ya nini unataka kifanyike mwilini mwako. Kama unahisi unachokwenda kukifanya sio “natural” na hujisikii vema kushiriki ngono Tigo basi acha/kataa kufanya hivyo.

-Mara mishipa ya Tigo ikitanuka kutokana na kufanywa huko mara kwa mara huwa haijirudi kama ilivyo kwenye uke kwa vile haikuumbwa kwa ajili ya shughuli hiyo.

-Wengi tunaamini kuwa kufanywa nyuma ni kwa mashoga tu lakini kuna wanawake wanafurahia kama ilivyo ngono ya mdomo na baadhi hujigeuza kama njia mbadala ya kuzuia mimba au kulinda bikira (zaidi ni ktk jamii ya waarabu).

-Ukizoea sana kupigwa nyuma na mishipa ya huko kutanuka, basi inasemekana kuwa utatatizwa wakati wa kujifungua/kuzaa, si hivyo tu bali unaweza ukawa na tatizo la kuvuja mkojo kwani hutoweza kukaza tena misuli yako ukeni ambayo hulegea baada ya kuzaa.
Swala muhimu sio kutisha watu bali kuwaelimisha na kuwaachia wao wachague mchele upi na pumba zipi. Ukiangalia yale yote yanayokatazwa au kuitwa miiko ndiyo yanayofanywa zaidi kuliko yale tunayoruhusiwa kuyazungumzia na kuyatenda.


*** binafsi napinga kwa nguvu zangu zote swala la Ngono kusiko (tigo) ila na heshimu chaguo/uamuzi wako…..wewe ndio mweye mwili na unafanya vile utakavyo.

Ushuri wa bure-Jiheshimu na thamini mwili wako…..usitoe tako lako kama dawa ya kumfanya mume asitoke nje au akupende zaidi…..ni aibu mumeo akikuta nyuma jamaa waliwahi pia.
Lazima tushikamane pamoja kukomesha tabia hii.


Thursday, October 3, 2013

Je Wajua shahawa huongeza uwe wa kupata mimba kwa mwanamke?


Wanasanyans wamesema ya kwamba manii(semen) yanayotolewa na mwanamume wakati wa kujamiana na mwanamke yanasaidia mwanamke kuwa na uwezo wa kushika mimba.Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa kimataifa chini ya Gregg Adams na kuchapishwa katika jarida la proceedings of the National Academy of Sciences, umesema ya kwamba manii sio tu hubeba shahawa (sperm) za mwanamume kwenda kwa mwanamke bali pia huchochea mayai ya mwanamke (ovaries) kutoa mayai ya uzazi.Protini inayopatikana katika shahawa inayojulikana kama Ovulation-Inducing Factor au IFO, ndio hasa huchochea sehemu ya ubongo inayojulikana kama hypothalamus kwenye ubongo wa mwanamke kutoa homoni ambazo hupelekwa moja kwa moja kwenye mfumo wa neva na kisha homoni hizo hupelekwa kwenye mfumo mwingine wa homoni unaojulikana kama endocrine system.Homoni hufika kwenye mfumo huu wa endocrine system kupitia sehemu ya ubongo inayojulikana kama pitituary gland na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa damu.Baada ya kufika wenye mzunguko wa damu, homoni hizi huenda moja kwa moja mpaka kwenye mayai ya mwanamke (ovary) na kuyachochea mayai haya kutoa mayai ya uzazi(ovum) katika hatua inayojulikana kama ovulation.
Watafiti hao wamesema wamegundua protini hii aina ya IFO katika shahawa za wanyama aina ya ilamas, sungura na hata kwa binadamu. Wanyama wengi wana viungo vya ziada vya kujamiana ambavyo hutoa manii kwenda kwenye shahawa lakini umuhimu wa manii hayo bado haujagundulika.
“Wazo la kuwa kuna chembechembe katika manii ya wanyama na binadamu ambayo huchochea ubongo wa mwanamke ni wazo geni kabisa, alisema Gregg Adams”.
Wanasayansi hao wameweza kugundua ya kwamba ni chembechembe hizi ndizo pia husaidia katika ukuaji, urekebishaji na ustawishaji wa seli za neva.
Katika utafiti huu ambao wanasayansi walitumia ngombe, ilamas na binadamu, wanasayansi hao waliweza kugundua protini aina ya Ovulation-Induced-Factor kutoka katika manii ya wanyama hawa pamoja na binadamu waliohusika katika utafiti huu.
Wanasayansi hao waliwachoma sindano yenye protini hii wanyama aina ya ilamas na kuwafanya wanyama hao kupata ovulation wakati walipowachoma ngombe sindano yenye protini hii aina ya IFO, ngombe hao walishindwa kuingia katika ovulation lakini protini hiyo iliweza kuwafanya ngombe kutengeza mifuko kwenye mayai yao ambayo ndio hasa hubeba mayai ya uzazi na hivyo kuwafanya ngome kuwa tayari kwa kushika mimba.Pia ilionekana ya kwamba protini hii (IFO) ina uwezo wa kustawisha mimba kwa ngombe hawa.
“Utafiti huu mpya unaongeza uelewa wetu wa mfumo wa ovulation lakini pia huongeza maswali mengi juu ya ovulation hiyo’, alisema Adams”
Tafiti zaidi zinahitajika ili kujua ni kazi gani ambayo protini hii aina ya IFO hufanya katika kumpa mtu uwezo wa kutunga au kushika mimba.Wanasayansi hao wanahisi uwepo wa protini hii kwa wingi kwa baadhi ya wanaume inawezekana ikawa ndio chanzo cha kuwafanya wanaume hao kuwa na uwezo mkubwa wa kutungisha mimba mwanamke (fertile).
Ovulation ni hatua ambayo yai la uzazi hutolewa na kwenda katika mfuko wa uzazi (uterus) na kusubiri shahawa ili lirutubishwe na kuwa mimba.Ovulation hii hutokea siku ya 14 baada ya mwanamke ya kuanza hedhi yake.Yai la uzazi ambalo hutolewa wakati huu hukaa kwa masaa 48 kusubiri kurutubishwa na kama halitarutubishwa na shahawa basi yai hili huharibika na kutolewa nje kama hedhi.Ni katika ovulation, ndio mwanamke huwa na uwezo/asilimia kubwa ya kushika ujauzito kama atajamiana na mwanamume.Dalili za ovulation ni pamoja na kichwa kuuma, kizunguzungu, kichefuchefu, matiti kuuma, kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini, kutokwa jasho kwa wingi usiku, kubadilika ladha ya ulimi, kuwa na hasira mara kwa mara, kupata hamu ya kujamiana, kutokwa na ute katika tupu ya mwanamke ,maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo

Friday, September 27, 2013

Oestradiol: Homoni zinazochochea ngono kwa wanawake

Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wa blog hii,ni muhimu ukashare na rafiki zako habari hii kama nilivyofanya nami katika kutupia macho huku na huko nimeona sio mbaya nikiwaletea wadau.
  • Wanawake wenye kiwango kikubwa cha vichocheo (homoni) aina ya oestradiol, wana mwamko mkubwa wa kushiriki tendo la ndoa kuliko wanawake wenzao wenye kiwango kidogo cha vichocheo hivyo.

Ni ajabu, wala si jambo la kawaida kwa wanawake walio wengi kujikuta katika matamanio, kiasi cha kujikuta wakilazimika kushiriki tendo la ndoa.Hata hivyo, homoni kadhaa zilizoko katika miili ya wengine zinawachochea kujitumbukiza kwenye tendo hilo.Utafiti wa baadhi ya wanasayansi umeonyesha kuwa baadhi yao wana kiwango kikubwa cha vichocheo mwili kinachoweza kushawishika kuwa na mpenzi wa nje au kumchoka haraka mwenza wake baada ya kuishi naye kwa kipindi fulani.Wanasayansi hao wamefanya uchunguzi na kugundua kuwa, wanawake wenye kiwango kikubwa cha vichocheo (homoni) aina ya oestradiol, wana mwamko mkubwa wa kushiriki tendo la ndoa kuliko wanawake wenzao wenye kiwango kidogo cha vichocheo hivyo.Vichocheo hivi aina ya oestradiol (oestrogen) ni vile  vinavyotumika katika kuzalisha mayai ya uzazi wa mwanamke. Pia, vichocheo hivyo ni vile ambavyo humpa mwanamke mwamko wa tendo la ndoa.Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Saikolojia nchini Uingereza walifanya utafiti kuhusu uhusiano uliopo kati ya vichocheo na tabia za watu na kubaini kuwa kiwango cha vichocheo  huweza kuelezea tabia ya mwanamke ikiwamo kumsababisha kuwa na tamaa za mwili zaidi tofauti na wanawake wengine.Wanasayansi hao, Dk Kristina Durante na Norm Li walitoa ushahidi wa utafiti wao kuwa mfumo wa kisaikolojia unachangia kwa kiasi kikubwa katika mwamko wa tendo la ndoa na tabia kwa wanawake.Wanawake  52 wenye umri wa kati ya miaka 17 na 30, wote wanafunzi wa vyuo vikuu walishiriki katika utafiti huo  na kuambiwa wasitumie njia yeyote ya uzazi wa mpango kwa sababu njia hizo huongeza vichocheo mwilini.Kwa upande wao, watafiti walipima kiwango cha homoni hizo kwa wanawake wote na walipewa maswali ya kujibu yaliyohusu mienendo yao ya kimapenzi, kutosheka na wenzao pamoja na uwezo wa kuvumilia kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani.Pia, washiriki hao walitakiwa kujibu maswali maalumu ambayo yanapima uwezekano wa washiriki hao kuwasaliti wenzao wao.Mwishowe, watafiti hao walibaini kuwa, wanawake wenye kiwango kikubwa cha vichocheo vya oestradiol wanapenda utani, wanapenda kupigana busu na ni rahisi kupata mwenza mpya wa kudumu wakati wowote.Matokeo yetu yalibaini kuwa, wanawake wenye kiwango kikubwa cha rutuba za uzazi hawatosheki na mwenza mmoja hasa waliyeishi naye kwa muda mrefu. Wana uwezo wa kutafuta mwenza mwingine anayewatosheleza,” alieleza Dk Durante.