Leo nimekuja na mada nyingine, kama kawaida ni mada nzuri itakayokupa ufahamu mpya juu ya maamuzi yako yahusuyo mapenzi. Hivi ni kweli kwamba unautendea haki moyo wako? Mpenzi uliyenaye unampenda au unajilazimisha tu kuwa naye?
Somo
la leo litakupa mwanga wa kujua haki ya moyo na tamaa za mwili wako ni
kipi sahihi kutendewa haki. Elewa kuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu
na kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi.
Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu
mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi
hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi.
Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haklupendi, yaani wewe
peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi! Kama ndivyo,
kwanini uwe mtumwa?
Unadhani
hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi
hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana,
huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!
Mapenzi
ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye
atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye
furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako!
Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!
Wakati
mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna
ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe,
umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini
ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!
Anatokea
mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi,
anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia
hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu
zangu!
Kama
mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu
yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako
ghafla. Hii inaama kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri
zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria
kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha!
KUJIFUNZA KUPENDA!
Baadhi
ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi,
lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa
lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. Hufanya hivyo ajidanganya kuwa
atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo.
"Pesa
anazo, magari anayo, hata kama simpendi nitajitahidi kumpenda
taratibu," baadhi ya wasichana huwaza hivi. Baada ya wazo hili kuingia
akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine
huweza kuingia katika ndoa.
MADHARA
Yapo
mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi wako uliyenaye.
Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndio
msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda,
unajihisi furaha na amani siku zote.
Madhara
makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume
mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea?
Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima
utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza
kukua.
UNATENDA HAKI?
Kamwe
usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni
jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo
linaewza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.
Kuwa
makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali
ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga
mustakabali wa maisha yako yajayo. CREDIT KWA JOSHUA
No comments:
Post a Comment