OMBA MSAMAHA KWA MPENZI WAKO:
Mpenzi
wangu naomba unisamehe, nakupenda sana dear na ni kweli kuna wakati
nakukosea, lakini amini nakupenda. Sijawahi kujuta na sitajuta kamwe
kuwa na wewe! Naamini nitaendelea kuwa mwaminifu kwako, sio leo tu, bali
siku zote za penzi letu!
*****
Tukae
kimya sheteni apite, naamini haikuwa akili yangu bali ni ushawishi wa
sheteni ambaye siku zote amekazania kuharibu penzi letu!
*****
Wewe
kwangu ni kila kitu, sipendi kuyaona machozi yako mpenzi wangu! Sogea
nikufute na unirudishe tena mikononi mwako, nakupenda sana dear!
*****
Wewe
ni taa kwangu imulikayo gizani, nakupenda sana mpenzi wangu wa moyo,
utakuwa wangu siku dear! Kosa nililofanya ni kwa bahati mbaya, naomba
unisamehe na ninaahidi kutorudia tena katika penzi letu!
*****
Tega
sikio dear, nakupenda sana, ukweli wa ile sms uliyoifuma kwenye simu
yangu, haikuwa yangu bali mtumaji alikosea kwa bahati mbaya! Nipo tayari
tumpigie tukiwa pamoja tumuulize, kweli niamini dear! Naomba usiniache
maana maisha yangu bila wewe ni sawa na giza nene!
****
Mimi kwako ni kipofu, nishike mkono tuvuke barabara, magari ni mengi na yanapita kwa kasi, siwezi kuona zaidi ya kusikia yakiunguruma, honi za magari siwezi kupima umbali wake, usiniache katikati ya barabara nitagongwa na kufa mara moja! Njoo niokoe nitagongwa mpenzi wangu! Forgive me dear...
No comments:
Post a Comment