Kula
nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi
katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali
kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema
kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi,
kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa
ya maziwa wazi.
Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika
maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na
mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati
huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.
Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana
na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi.
Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya
wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu
huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta
mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi
kimoja kikubwa sana.
Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi
kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama
hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi
huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama
mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani
wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa
sana.
Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata
maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi
mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama
anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa,
ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama
wanaume.
No comments:
Post a Comment