Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wa blog hii,ni muhimu ukashare na rafiki zako habari hii kama nilivyofanya nami katika kutupia macho huku na huko nimeona sio mbaya nikiwaletea wadau.
- Wanawake wenye kiwango kikubwa cha
vichocheo (homoni) aina ya oestradiol, wana mwamko mkubwa wa kushiriki
tendo la ndoa kuliko wanawake wenzao wenye kiwango kidogo cha vichocheo
hivyo.
Ni ajabu, wala si jambo la kawaida kwa wanawake
walio wengi kujikuta katika matamanio, kiasi cha kujikuta wakilazimika
kushiriki tendo la ndoa.Hata hivyo, homoni kadhaa zilizoko katika miili ya wengine zinawachochea kujitumbukiza kwenye tendo hilo.Utafiti wa baadhi ya wanasayansi umeonyesha kuwa
baadhi yao wana kiwango kikubwa cha vichocheo mwili kinachoweza
kushawishika kuwa na mpenzi wa nje au kumchoka haraka mwenza wake baada
ya kuishi naye kwa kipindi fulani.Wanasayansi hao wamefanya uchunguzi na kugundua
kuwa, wanawake wenye kiwango kikubwa cha vichocheo (homoni) aina ya
oestradiol, wana mwamko mkubwa wa kushiriki tendo la ndoa kuliko
wanawake wenzao wenye kiwango kidogo cha vichocheo hivyo.Vichocheo hivi aina ya oestradiol (oestrogen) ni
vile vinavyotumika katika kuzalisha mayai ya uzazi wa mwanamke. Pia,
vichocheo hivyo ni vile ambavyo humpa mwanamke mwamko wa tendo la ndoa.Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Saikolojia nchini
Uingereza walifanya utafiti kuhusu uhusiano uliopo kati ya vichocheo na
tabia za watu na kubaini kuwa kiwango cha vichocheo huweza kuelezea
tabia ya mwanamke ikiwamo kumsababisha kuwa na tamaa za mwili zaidi
tofauti na wanawake wengine.Wanasayansi hao, Dk Kristina Durante na Norm Li
walitoa ushahidi wa utafiti wao kuwa mfumo wa kisaikolojia unachangia
kwa kiasi kikubwa katika mwamko wa tendo la ndoa na tabia kwa wanawake.Wanawake 52 wenye umri wa kati ya miaka 17 na 30,
wote wanafunzi wa vyuo vikuu walishiriki katika utafiti huo na
kuambiwa wasitumie njia yeyote ya uzazi wa mpango kwa sababu njia hizo
huongeza vichocheo mwilini.Kwa upande wao, watafiti walipima kiwango cha
homoni hizo kwa wanawake wote na walipewa maswali ya kujibu yaliyohusu
mienendo yao ya kimapenzi, kutosheka na wenzao pamoja na uwezo wa
kuvumilia kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani.Pia, washiriki hao walitakiwa kujibu maswali maalumu ambayo yanapima uwezekano wa washiriki hao kuwasaliti wenzao wao.Mwishowe, watafiti hao walibaini kuwa, wanawake
wenye kiwango kikubwa cha vichocheo vya oestradiol wanapenda utani,
wanapenda kupigana busu na ni rahisi kupata mwenza mpya wa kudumu wakati
wowote.Matokeo yetu yalibaini kuwa, wanawake wenye
kiwango kikubwa cha rutuba za uzazi hawatosheki na mwenza mmoja hasa
waliyeishi naye kwa muda mrefu. Wana uwezo wa kutafuta mwenza mwingine
anayewatosheleza,” alieleza Dk Durante.
No comments:
Post a Comment