Saturday, September 7, 2013

Wanawake kujilinganisha na wanaume ni sign ya low self esteem

Self esteem ni hali ya kisaikolojia inayomuonyesha mtu jinsi gani anavyojitambua na kujikubali. Mtu mwenye self esteem ya juu, anakuwa ni mtu jasiri, anayejikubali, anajitambua, anajiamini na hana shida na alivyoumbwa. Kuwa mfupi au mrefu, mweusi au mweupe, maskini au tajiri, mwanaume au mwanamke, si kitu kinaweza kumsumbua mtu yeyote ambaye self esteem yake iko vizuri. Unapoona una shida ya kujikubali au umbo lako, au jinsia yako au hali yako ya maisha ujue shida si hicho unachokiona bali shida iko ndani yako. Ndio maana unaona kuna matajiri wengi tu unaona hawajikubali wala kuridhika, wakati kuna mtu ana bajaj tu na anaenjoy maisha yake. Utaona kuna mtu ana nafasi yake kubwa tu kiajira, au kwenye siasa lakini hajawahi kuridhika. Mtu mwenye shida hii hata kumpa kutawala dunia ataona kuwa bado kuna kitu hakiko sawa. Ni kwa maelezo hayo naomba niwaambie wananwake wenzangu ukiona kila mara, unapenda kujilinganisha na kaka zako, au mume wako, na kuona kuna kitu kinapungua hata ungeumbwa mwanaume ungetamani uwe mwanamke.       Jifunze kujikubali ulivyo, na kujifurahia kutoka ndani ya nafsi yako, jifunze kuridhika na ulicho nacho kwa sasa(materials) ukiendelea kuongezea kidogo kidogo, na usijali sana mtazamo wa dunia juu yako, maana kuridhika kwa ukweli kunaanzia wewe mwenyewe unavyojiona.

No comments:

Post a Comment