Friday, August 30, 2013

Mwanamke hujenga Imani zaidi kwa Mtu ampaye Kumbatio (hug)



Inaaminika kuwa mwanamke hujenga imani zaidi kwa mtu ampaye kumbatio. Haya ni matokeo baada ya tafiti zilizofanywa na wataalamu wa mambo ya mahusiano na tabia huko ng'ambo.

Inasemekana kuwa ukitaka kuaminiwa na mwanamke kirahisi, basi kumbatio ni moja ya njia ambayo humsababisha mwanamke kukujengea zaidi hali ya kukuamini.

Na utafiti huo ukaenda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa, walau muda wa kumbatio uwe karibia sekunde 15.(Kama waziona ni ndogo au nyingi just try to count from 1 to 15 in an interval of a second).

Onyo:
Kwa sisi wanaume kabla hujampa kumbatio mdada au mwanamke jaribu kuzingati mambo kadhaa...
1. Hakikisha mwili wako ni msafi hautoi harufu mbaya.
2. Hakikisha hautokwi na majasho.
3. Ambatanisha na tabasamu,ikiwezekana mnong'oneze rafikiyo/mpenzio maneno matamu.

No comments:

Post a Comment