Wafuatiliaji wa tabia na mienendo ya wanawake wamegundua ya kwamba wanawake hufurahia suala la kwenda kufanya manunuzi kama mtu afurahiavyo kwenda shereheni.
Sio kwamba huwa wanafanya tu manunuzi, lakini lazima watenge muda wa kunywa kahawa kidogo, kupata bites za hapa na pale n.k.
Hizi zifuatazo ni tabia kwa uchache tu wazioneshazo kina mama wawapo 'shopping', na ndio ambazo hupoteza sana muda:
1. Wanawake wanapoenda kufanya manunuzi hupendelea kuambatana na mlolongo wa marafiki.
2. Hupenda kugusa hiki mara kile hata kama hawatanunua, na usiombe waingie duka la vipodozi haswa uturi 'perfumes'.
3. Ni wagumu wa kufikia maamuzi ya haraka juu ya kipi wachukue kipi waache, kifupi ni kwamba huwa hawawezi.
4. Wapo makini sana kuchunguza kitu katika kila nyanja 'aspect'...Mara wataangalia rangi, bei, saizi na ni namna gani kitu hicho kitafaa kikiwekwa mwilini au mahali fulani.
5. Mwanamke anapoenda manunuzi sio kwamba anataka kujifurahisha yeye tu kwa kile anachokinunua, mara nyingi atapenda na marafiki zake wakikubali.
6. Hutumia muda mrefu sana kwenye kujaribu, mathalani kama ni nguo basi itavaliwa mara tatu tatu hadi aridhike.
7. Wanawake wanapenda sana kupunguziwa bei 'bargaining', yaani hapa ndio wanapopoteza muda mrefu.
No comments:
Post a Comment