Habari zenu wadau
Kila Mtu Maishani kwake anaye mpenzi wake wa kwanza. Kuna walio na bahati ya kuwa na wapenzi wao wa mwanzo mpaka leo na wengine wapo katika ndoa zao. Mungu awape kila la kheri. Ila tupo wa kina sisi, tulishapendaga saana zamani, kwa bahati mbaya hatukurudishiwa upendo wa kiwango sawa na hao tuliowapenda kwa moyo woote, na leo tupo katika mahusiano mengine. Kuna uwezekano miongoni mwetu tumeshawasahau hao tulio wapenda kwani Mungu ameshatupa mahusiano mengine ambayo ni bora na matamu zaidi kiasi kwamba hatuna hata hamu ya kuyafikiria ya nyuma. Ila pia tupo katika sisi, japokuwa tupo katika mahusiano mengine, lakini kila siku tunawakumbuka wenza wetu wa awali, tunajutia katika nafsi zetu kwanini hatupo nao, na kama tutapewa nafasi ya kuomba kitu kwa Mungu na kukubaliwa basi leo hii tungeomba kuwa pamoja na wenza wetu, Wapenzi wetu wa Mara ya Kwanza.
Haimaanishi Mpenzi wa kwanza awe ni yule aliyemtua Bikira Mwanamke au aliyekuwa wa kwanza kufanya mapenzi na mwanamke, hapana, hapa namzungumzia Mpenzi yule ambaye aliuteka moyo wako wote, roho, akili na nafsi, yeye ndo akawa kila kitu kwako, bora usile yeye ale, yule aliyekufanya Chozi likakutoka kwa ajili yake, yule ambaye ukianza kuelezea ni jinsi gani una hisia kwake basi utamaliza vitabu na wino na bado ukawa na la kuzndika........
Kuna Kisa kimetokea maeneo fulani ambapo wamefumaniwa watu wazima wakifanya mapenzi katika nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake. Walipokamatwa na raia wema katika utetezi wao nimepata jambo la kutahadharisha. Jamaa alisema kwamba "Huyu mwanamke mimi ndio mwanaume wake wa kwanza, nnampenda ingawa kwa sasa ameolewa, ni muda mrefu hatujaonana, leo kama bahati nimekutana nae maeneo haya halafu sina hela ya kwenda "Guest" ndo maana tumeona tuje hapa tujienzi"
Hapa nikajiuliza, ingekuwa mimi au wewe ungefanyaje, mwenza wako kateleza au wewe mwenyewe ndo umeteleza hivyo? Ukweli ni kwamba Kama kweli tuliwapenda Wapenzi wetu wa Kwanza, inakuwa vigumu kuwagomea au kuwakatalia wanapokuwa na ushawishi juu yetu, hasa pale inapotokea tumepoteana kwa muda mrefu. Kwa vile tayari tupo katika mahusiano mengine, yatupasa tuwaheshimu wenza wetu tuliokuwa nao sasa kwani wameamua kuwaacha wote na kuwa na sisi, Tuwaheshimu, Tuwaonee Huruma na Tujiheshimu wenyewe. Pia tujitahidi kuwa mbali nao kadri na zaidi ya Uwezo Wetu.
No comments:
Post a Comment