Wednesday, October 16, 2013

MAPENZI YA OFISINI HUVURUGA SAIKOLOJI YA MTU.

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.

Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.

Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi kimoja kikubwa sana.

Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa sana.

Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.

No comments:

Post a Comment