Friday, October 4, 2013

MADHARA YA KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE

     Habari ndugu mdau wa blog hii,natumaini upo poa na unapendezewa na post zetu,leo tugusie madhara ya kuruka ukuta yaani ngono ya kinyume na maumbile.

Tunapoamua kufanya jambo sio kwamba tunafuata mkumbo au kulazimishwa bali ni our choice.
Kufanya ngono kusiko a.k.a Tigo “MWIKO” katika jamii nyingi Ulimwenguni sio kwa vile tu inamaanika kuwa ni uchafu na inamadhara makubwa ya kimwili, kiakili na kiafya bali ni kinyume na mafundisho ya imani zetu za Dini.

Kinachofanyika chumbani ni uamuzi wenu ninyi wawili mnaopendana ikiwa tu mtakubaliana na kufanya hivo na pia ni siri yako wewe na mpenzi wako, kuna wapenzi wengi tunafanya mambo ya ajabu sana na watu tunaowapenda na tunafurahia na tunazidi kupendana na kutakana zaidi na zaidi kila siku….lakini mambo hayo ni “taboo” ktk jamii kama ilivyo kwa Tigo 

Kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) hujaribu na kisha wanajikuta wanafurahia na hivyo wanaendelea na kuna wengine hutaka kujua “unajisikiaje” lakini wanajikuta hawafurahii au mmoja wao hafurahii na hivyo wanaacha na kutorudia tena tendo hilo la mugongo-mugongo.
Pamoja na kuwa watu kuheshimu miiko ya dini zao, kupinga na kulisema vibaya tendo hili wachunguzi wa mambo ya Tigo wanadai kuwa mwanamke mmoja kati ya wanne anashiriki ngono ya nyuma (sasa hii sijui ni kuridhisha wapenzi au ni wao wanafurahia)…….wazoefu watusaidie hapa.

Ukweli kuhusu Tigo.- Sio tendo asilia ktk swala zima la ngono na mapenzi hivyo kumbuka unapoamua kugawa tako kuwa na uhakika ndio kitu unataka kukifanya na sio kukifanya kwa vile “mchumba” kaomba/anataka…..wewe ndio mwenye maamuzi makuu ya nini unataka kifanyike mwilini mwako. Kama unahisi unachokwenda kukifanya sio “natural” na hujisikii vema kushiriki ngono Tigo basi acha/kataa kufanya hivyo.

-Mara mishipa ya Tigo ikitanuka kutokana na kufanywa huko mara kwa mara huwa haijirudi kama ilivyo kwenye uke kwa vile haikuumbwa kwa ajili ya shughuli hiyo.

-Wengi tunaamini kuwa kufanywa nyuma ni kwa mashoga tu lakini kuna wanawake wanafurahia kama ilivyo ngono ya mdomo na baadhi hujigeuza kama njia mbadala ya kuzuia mimba au kulinda bikira (zaidi ni ktk jamii ya waarabu).

-Ukizoea sana kupigwa nyuma na mishipa ya huko kutanuka, basi inasemekana kuwa utatatizwa wakati wa kujifungua/kuzaa, si hivyo tu bali unaweza ukawa na tatizo la kuvuja mkojo kwani hutoweza kukaza tena misuli yako ukeni ambayo hulegea baada ya kuzaa.
Swala muhimu sio kutisha watu bali kuwaelimisha na kuwaachia wao wachague mchele upi na pumba zipi. Ukiangalia yale yote yanayokatazwa au kuitwa miiko ndiyo yanayofanywa zaidi kuliko yale tunayoruhusiwa kuyazungumzia na kuyatenda.


*** binafsi napinga kwa nguvu zangu zote swala la Ngono kusiko (tigo) ila na heshimu chaguo/uamuzi wako…..wewe ndio mweye mwili na unafanya vile utakavyo.

Ushuri wa bure-Jiheshimu na thamini mwili wako…..usitoe tako lako kama dawa ya kumfanya mume asitoke nje au akupende zaidi…..ni aibu mumeo akikuta nyuma jamaa waliwahi pia.
Lazima tushikamane pamoja kukomesha tabia hii.


No comments:

Post a Comment