Tuesday, September 10, 2013

MAMBO MATANO YA KUJARIBU WIKI HII!!!


Wakati mwingine si lazima kufanya mapenzi ili kujenga ukaribu na mpenzi wako. Unaweza kuviona kama vitu vidogo sana na labda vinaweza kutokuwa na umuhimu wowote, ila kumbuka ya kuwa kwenye mapenzi ni vile vidogo ndio viletavyo tofauti kubwa sana.

Mara nyingi wale wapenzi waliokaa muda mrefu pamoja hujikuta wakipuuzia vitu vya namna hii kwasababu wanahisi hawana haja ya kuvifanya, me ningeshauri mjaribu just for this week alafu muone wenyewe tofauti itakayojitokeza kwenye maisha yenu ya kimapenzi.





(1) Walk on the beach



Ni vyema kutafuta ufukwe ambao uko kimya na una mandhari nzuri inayo vutia ili kuspend time na mpenzi wako. Mjaribu kucheza kwa furaha, mkishare vinywaji na kuzikumbuka zile siku mlizoanza mapenzi yenu. Bila kusahau kupeana mabusu matamu matamu ili kutimiza haswa nia ya kuwa na a romantic walk on the beach.


(2) Trade nightly foot rubs



Ni rahisi, pia intimate na pia huleta hisia nzuri sana. Wakati mwingine mambo yanaweza yasiende vizuri pale mtu unaporudi umechoka na miguu inauma kutokana na pirika pirika za kutafuta maisha. Miguu kuuma kunaweza sababisha mtu ukashindwa hata kuenjoy usiku mzuri wa kimahaba. Mfanyie mpenzi wako massage ya miguu kwa kutumia mafuta mazuri na laini na yenye manukato mazuri na pia muombe na yeye akufanyie huku mkiongea mambo mazuri ya kimahaba au kukumbushiana zile siku mlizoenjoy kupita kiasi katika maisha yenu ya kimahaba. Inaweza tokea mkafanya zaidi ya foot rubs na kujikuta mnatengeneza kumbukumbu nyingine ya kimahaba.


(3) Sharing a bubble bath with an extra touch



Hii ni njia nzuri na bora ya kurelax baada ya siku iliojaa kazi ngumu( pia inaweza safisha njia kwa usiku uliojaa mahaba mazito) kwa kushare a romantic bubble bath. Maandalizi madogo tu yanahitajika, a short trip kwenye supermaket na kununua mishumaa yenye marashi pamoja na jell za kuogea nzuri ambazo zina marashi mazuri na ni special kwaajili ya bubble bathing. Kinachofuata hapo ni kuviandaa(unaweza ongezea roses kama hapo kwenye picha) na kushare na mpenzi wako huku mkiongelea mambo ya kimahaba na kushare vinywaji na vicheko pamoja.

(4) Prepare dinner for your lover


Kwanza ningependa kuwapa challenge wakinakaka cause najua wakinadada hili wanaweza kulifanya bila matatizo. Si lazima uwe mpishi mzuri, unaweza tu kuwa mpishi wa kawaida, ila, ile nia ya wewe kumuandalia mpenzi wako dinner yenye a very romantic setup inatosha kwake yeye kuappreciate effort yote ulioifanya na kuongeza ukaribu kati yenu.

Jitahidi na kupitia vitabu vya mapishi ili upate kile ambacho utaweza kukiandaa kwa urahisi, kisha, siku moja fanya maandalizi kwa kununua wine nzuri ambayo haitowalewesha na itakayoongeza utamu wa chakula utakachokiandaa, mishumaa na roses, pia andaa sehemu katika nyumba yenu ambayo unajua itakuwa ya muafaka na ipambe kwa mishumaa na roses na meza ya kulia chakula kwaajili ya watu wawili, hakikisha asilimia kubwa ya mwamnga itoke kwenye mishumaa iliyowashwa. Kinachofuata hakiitaji mimi kuelezea....


(5) Write a steamy love letter to your lover



Take your time kuweka mawazo yako kwenye hiyo barua kabla ya kuiwasilisha kwa mpenzi wako. Ifanye barua hiyo kuwa na muonekano wa kimahaba kadri ya uwezo wako. Elezea kwa kina na kwa ufafanuzi wa kimahaba vile vitu vyote vinavyokuvutia kutoka kwa mpenzi wako. 



Toa mapendekezo ya sehemu ya kukutana na mpenzi wako na elezea kile kitakachotokea kwa kimahaba zaidi. Hakikisha unakuwa muwazi kuhusu muda na tarehe ambayo unataka mkutane na mpenzi wako, pia hakikisha wote mtakuwa huru hiyo siku kwa kuspend time pamoja. 

Mwisho kabisa wa barua mweleweshe mpenzi wako kuwa asiongelee hili jambo matakapokuwa pamoja atakaporudi nyumbani au hata mkiwasiliana kwenye simu. Hii itasaidia kuongeza mzuka wa kimahaba na kumfanya aisubirie hiyo siku kwa hamu na pia itasaidia yeye kufanya juu chini kutoikosa hiyo siku.

Kwa kumalizai, ipulizie perfume yako uipendayo na ambayo unajua mpenzi wako ataitambua au unaweza kuifanyia chochote ambacho kitakutambulisha wewe pale mpenzi wako atakapoisoma. Unaweza kumpelekea wewe mwenyewe kama anafanya kazi karibu au kama amesafiri, wakati unamsaidia kupack mizigo yake iweke mahala ambapo ataweza kuiona kirahisi pale atakapofika kwenye safari yake.

No comments:

Post a Comment