Monday, March 11, 2013

TABIA MBAYA ZA MUME ZINAWEZA KUBADILI MSIMAMO MZURI WA MKE?




Leo tuongee wapendwa wangu,Inasemekana kuwa baadh ya tabia za wanawake walio wengi huwa ni nzuri
sana, kipindi cha mwanzo na hasa katika upande wa mapenzi, lakin kadri siku zinavyozidi kwenda, mambo
hubadilika na kuwa kinyume, wanaume wanabadili tabia kiasi cha mke kujuta kwanini aliolewa,

Katika kupekua pekua kwangu,nimeikuta kitabu hiki, kimenivutia na nimeamini ni kweli kabisa,
nimeileta kwenu tufundishane,kitabu kimeandikwa
75% of woman’s are in loveless and lifeless marriages

Wanaume wengi sana huficha makucha yapo wanapotaka kuoa,hujifanya wastaarab sana, lakini
baada ya ndoa kufika miaka 2 au 3 mambo huenda ndivyo sivyo, unakuta mwanaume amekosea
kosa ambalo hata mtoto akiona anajua kweli baba kakosea, lakini wanaume wanjifanya Manunda, hawakubali makosa, wala nini

Mbaya zaidi atakapoanza mahusiano nje ya ndoa, uaminifu hakuna tena, gubu mara kwa
mara, anaweza lala vizuri, akaamka amenuna, au anaweza fanya mambo kwa siri bila hata
kukushirikisha mkewe.

Na hata ukimkamata kwa hicho cha sirialichokifanya, bado anaweza kuwa mbishi na kukugeuzia kibao, na unaweza kuthibitisha pia, lakini bado akajifanya mbishi, ah!~ tabia hii inakera sana jamani tena bila hata haya wengine hudiriki kuongea na simu za wanawake zao hata mbele yako, ukiuliza unajibiwa, mfanyakazi mwenzangu, wakati unaona dalili zote kuwa ni simu ya mapenzi

Mwingine anaweza kuanza hata kumdunda mkewe, kwa sababu za kipuuzi, au kama akiuziwa huko nje na wanawake zake basi hasira zake zoote zinakuja kuishia kwa watoto, sasa ndio maisha gani hayo jamani?

Yote tisa, kumi akichukia eti hata matumiz ya familia haachi, Sasa je, kwa haya yote na mengine
unayoyajua wewe, ni kweli yanachangia 99% kubadili tabia nzuri au msimamo alionao mkewe?

Wanawake wanapenda sana kupendwa, kubembelezwa,
kuelekezwa kwa utaratibu, kusifiwa, na kuheshimiwa sana na waume zetu, hali inayopelekea msimamo wa mwanamke kuwa imara zaidi, na vipi kama ukivikosa
vyote hivyo kwa mumeo?

kila wakati umekua mtu wa kujuta,kulia, na huna furaha, sasa hali hii inaweza kubadili tabia yako na kutamani kufanya yasiyostahili???

No comments:

Post a Comment